Duration 13:20

WAZIRI GWAJIMA, DKT MOLLEL WATENGENEZA DAWA TIBA ASILI NA KUINYWA NANI KASEMA SINYWI, SIJIFUKIZI

85 023 watched
0
522
Published 1 Feb 2021

WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na Watoto imewataka wananchi kuchukua tahadhari ikiwamo matumizi ya dawa za tiba asili zilizothibitishwa na maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali dhidi mlipuko wa awamu ya pili wa ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya CORONA unaoripotiwa kuenea katika nchi za Jirani. Akitoa ufafanuzi kwa wanahabari jijini Dodoma kuhusu kujikinga na Magonjwa ya Kuambukiza na Yasiyoambukiza waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa hayo na kwamba haipo tayari kupokea chanjo yoyote na badala yake wananchi watumie dawa za tiba asili zilizothibitishwa. Aidha akatumia wasaa huo kutoa maelekezo kwa Baraza la Tiba Asili nchini kutoa orodha ya Dawa zote zilizoidhinishwa chini ya Utaratibu unaoihusisha maabara ya Mkemia Mkuu. Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akasisitiza wananchi kutopuuzia matumizi ya dawa asili kwa kuwa zimekuwa zikitumika tangu enzi na enzi hata kabla ya uwepo wa Ugonjwa wa COVID 19

Category

Show more

Comments - 442