Duration 1:28:17

NDOTO NA SIKU ZETU: BISHOP GWAJIMA IS LIVE NOW: 02.08.2020

44 244 watched
0
468
Published 2 Aug 2020

TAREHE 02.08.2020 SOMO: NDOTO NA SIKU ZETU -Kwenye Biblia kuna ndoto 21 kwanini waota ndoto ni wachache lakini ndoto ni nyingi kwasababu MUNGU ANAZUNGU MZA NA WATU KUPITIA NDOTO. SABABU ZA KUOTA NDOTO ZINAZO JIRUDIA -Mungu anaongea na watu kupitia ndoto. Anaweza kuongea na wewe hata mara tatu kama ujatendea kazi kile alicho ongea na wewe kupitia ndoto. ‭‭MHUBIRI‬ ‭1:3‬ “Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?” 1/ Ndoto huja kwa wingi wa shuhuri hunazo zifanya 2/ jambo unaliota lime hakikishwa -Mungu haluhusu matatizo ya kupate, Mungu ana kutengeneza wewe ili upigane vita na maadui wote wanao kufatilia. -Mungu akitaka kukupigania anakupa nguvu za kupigana katika vita itakayo kuja kukukabili. -Kuna kazi zingine hazi wezi kutokea mpaka ufunge na kuomba . KUNA NDOTO WA KATI WA ANAGO LA KALE NA KUNA NDOTO WA KATI WA AGANO JIPYA ‭‭MWANZO‬ ‭20:1-3‬ “Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari. Ibrahimu akamnena Sara mkewe, Huyu ni ndugu yangu. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akapeleka watu akamtwaa Sara. Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.”‬‬ -Neno ndoto limeanzia kwenye kitabu cha mwanzo -Unapo otandoto siokwamba ndio inatokea wakati huohuo, Ndoto huja kama taarifa juu ya jambo fulani litakalo tokea siku au wakati ujao. -Kwenye agano la kale unapo ota ndoto siokwamba litatokea ‭‭MWANZO ‭40:1-9‬ “Ikawa, baada ya mambo hayo, mnyweshaji wa mfalme wa Misri, na mwokaji wake, wakamkosa bwana wao, mfalme wa Misri. Farao akawaghadhibikia maakida wake wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji. Akawatia katika lindo nyumbani mwa mkuu wa askari, humo gerezani, mahali alipofungwa Yusufu. Mkuu wa askari akamwekea Yusufu watu hao, naye akawahudumu, nao wakakaa siku kadha wa kadha katika kifungo. Wakaota ndoto wote wawili, kila mtu ndoto yake usiku mmoja, kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake, mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliofungwa gerezani. Yusufu akawajia asubuhi, akawaona wamefadhaika. Akawauliza hao maakida wa Farao, waliokuwa pamoja naye katika kifungo, nyumbani mwa bwana wake, akisema, Mbona nyuso zenu zimekunjamana leo? Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Kufasiri si kazi ya Mungu? Tafadhalini mniambie. Mnyweshaji mkuu akamhadithia Yusufu ndoto yake; akamwambia, Katika ndoto yangu nimeota, uko mzabibu mbele yangu. -Kwenye kitabu cha Mwanzo kuna story za watu wa wili waliota ndoto nao ni Mkuu wa mwokaji na mkuu wa mnyweshaji. -Unapo ota ndoto unapewa talifa juu ya jambo fulani linalo kuja kutokea baada ya siku tatu ,wiki , mwezi au mwaka kabisa.Kila mtu na ndoto yake -Ndoto huja kama talifa juu ya jambo fulani ambayo halijatokea ila Mungu anakupa tarifa juu ya jambo litakalo kuja kutokea ili ulitendee kazi. -Ukiota ndoto ambayo haina fomura basi hakika hiyo ndoto itatokea kwa siku chache zijazo. Nakama ukiota ndoto alfu aijatokea ujue kuna mchoro Rohono -Ndoto za zamani zilikua zinatokea lakini ndoto za saivi zina tabiliwa. -Ndoto utafasiliwa kwa utulivu ndoto - Ndoto ya agano jipya inaanza ivi Yusufu alikuwa mwenye haki ndio maana hakumuabisha Mariam, ndipo akatokewa na malaika kwenye ndoto KANUNI 5 ZA NDOTO: 1/Ndoto lazima iwe kubwa kuliko uwezo wako wa kimwili 2/Ndoto inayotoka kwa Mungu lazima iwe ya kutisha 3/Ndoto ndogo haitokagi kwa Mungu 4/Ndogo ya Mungu huwa ni kubwa sana 5/Muota ndoto hafi -Ndoto ya mtu ndani yake ni mapenzi Mungu. Kwenye Agano jipya unaweza kuota ndoto na ukaibadilisha. -Ndoto kwenye agano jipya unaweza kuiepuka kama ilivyo pangwa -Unailetaje ndoto kwenye maisha haya tunayo ishi. Ndoto tunzo ota ni tofauti na za kwenye Biblia. AGANO JIPYA NA SAIVI NI TOFAUTI: -Unapokua umelala wachawi wana kuja wakiwa wamejibadirisha maumbo yao na kutumia maumbo ya watu wengine ili kukujia katika ndoto na kutimiza wanacho kitaka. -Ukiwa umelala kila jambo linalo tokea uendeshwa katika ulimwengu wa Rohoni ndio maana mchawi akija kwako anajibadirisha umbolake. -Kwenye ulimwengu wa Roho kila jambo linalokuwa linaendelea na kufanyika huwa linafanyika katika ulimwengu wa Roho. KUNA AINA TATU (3) ZA MARAFIKI. 1/ Confidant 2/Constituents 3/ Comrades -Mungu huya beba maneno ya watu wake na kuya timiza. -Kila jambo na wakati wake kuna wa kati wa kutupa mawe, kuna wakati wa kukusanya mawe, kuna wakati wa kulia na kuna wakati wakucheka.

Category

Show more

Comments - 154